MHANDISI WA MAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA ASHIKILIWA POLISI KWA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA MRADI
tarehe 21-09-2017
KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA GERMIN MUSHI |
Jeshi la polisi katika wilaya ya Mbinga mkoani
Ruvuma linamshikia mhandisi wa maji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga Bi
Vivian Ndolwa kwa tuhuma za kuhusika na ubadhirifu wa fedha za mradi wa maji
zaidi ya shilingi milioni mia saba.
Akidhibitisha kushikiliwa kwa mahandisi huyo kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma SACP Germin Mushi amesema kuwa mtuhumiwa huyo
alikamatwa Sept 19 mwaka huu,ambapo amesema kuwa mhandisi huyo alikuwa
akisimamia mradi wa maji wa katika kitongoji cha Mnazi mmoja kijiji cha Mkako
kata ya Mkako mmkoani humo.
Kamanda Mushi amesema kuwa,mradi huo unaofadhiliwa
na benki ya dunia ulitakiwa kukamilika March 28 2014 lakini hadi sasa mradi huo
haujakamilika na umejengwa chini ya kiwango hivyo wameamua kumkamata ili akjibu
tuhuma hizo zinazomkabili.
Hata hivyo amesema baada ya kukamilika kwa upelelezi
jalada la kesi litapelekwa kwa mwanasheria wa serikali wa mkoa wa Ruvuma kwa
hatua zaidi.
MHANDISI WA MAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA ASHIKILIWA POLISI KWA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA MRADI
Reviewed by safina radio
on
September 21, 2017
Rating:
No comments