ROONEY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUENDESHA GARI AKIWA AME LEWA



TAREHE 18-09-2017
 WAYNE ROONEY 
Nahodha wa zamani wa kikosi cha England Wayne Rooney amefika mahakamani na kukiri kuendesha gari akiwa mlevi.
Alikamatwa wakati polisi walisimamisha gari lake huko Wilmslow, Cheshire tarehe mosi mwezi Septemba.
Rooney 31 alipigwa marufuku ya kuendesha gari kwa miaka miwili na kuamrishwa kutoa huduma ya jamii bila malipo kwa masaa 100.
Rooney pia aliamrishwa kulipa pauni 170 wakati alifika katika mahakama ya Stockport.
Mzaliwa huyo wa Liverpool aliyejiunga tena na klabu yake ya utotoni ya Eveton miaka 13 tangu akihame na kuelekea Manchester United.

Baba huyo wa watoto watatu ndiye anayeshikisa rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi nchini Uingereza.
ROONEY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUENDESHA GARI AKIWA AME LEWA ROONEY  AFIKISHWA   MAHAKAMANI   KWA  KOSA  LA   KUENDESHA  GARI  AKIWA  AME LEWA Reviewed by safina radio on September 18, 2017 Rating: 5

No comments