IMEELEZWA KUWA VITENDO VYA RUSHWA VINAENDELEA KUPUNGUA HAPA NCHINI


TAREHE 21-09-2017

NAIBU MKURUGENZI TAKUKURU BRIGEDIA JENERALI  JOHN  MBUNGO

Naibu mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) hapa nchini, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema kuwa vitendo vya rushwa vinaendelea kupungua hapa nchini kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na taasisi hiyo ya kuwakamata na kuwachukulia hatua wala rushwa.


Jenerali Mbungo ameyasema hayo jijini Dar-es-salaam,wakati akifungua mafunzo ya namna ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa viongozi wa serikali za mitaa na wakurugenzi wa taasisi na mashirika mbalimbali ya mkoa wa Dar-es-salaam ambamo ndipo panapofanyika shughuli nyingi za wananchi.

Amesema kuwa mafunzo hayo ni mwendelezo wa utaratibu wa takukuru ya kuwafundisha watoa huduma namna ya kuzuia na kupambana na rushwa katika maeneo yao ya kazi ikiwemo polisi na mahakamani,hivyo baada ya mafunzo hayo wanaamini kuwa rushwa itapungua kwa kiasi kikubwa katika maeneo mbalimbali ya kuhudumia wananchi hapa nchini.


Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Dar-es-salaam Bi Theresia Mbando amesema kuwa,katika mkoa huo vitendo vya rushwa vimepungua katika maeneo ya kutolea huduma,ambapo pia amewataka watoa huduma wa mkoa huo kuzingatia maadili ya kazi na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
IMEELEZWA KUWA VITENDO VYA RUSHWA VINAENDELEA KUPUNGUA HAPA NCHINI IMEELEZWA   KUWA   VITENDO   VYA   RUSHWA  VINAENDELEA  KUPUNGUA  HAPA  NCHINI Reviewed by safina radio on September 21, 2017 Rating: 5

No comments