WAMAMA WAJAWAZITO 100 WAMEFARIKI DUNIA MKOANI MWANZA TANGU MWEZI JANUARI HADI AGOSTI MWAKA HUU




TAREHE 20-09-2017

BAADHI   YA  WAMAMA WAJAWAZITO WAKIWA  KATIKA KITUO CHA AFYA

Imeelezwa kuwa Jumla ya wamama wajawzito 100 wamefariki dunia mkoani Mwanza kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Agosti mwaka huu kutokana na matatizo ya uzazi ikilinganishwa na vifo vya akina mama wajawazito 80 waliofariki dunia mwaka jana katika kipindi kama hicho.

Hayo yameelezwa na mratibu wa afya wa mama na mtoto mkoani Mwanza Bi Cesilia Mrema,ambapo amesema kuwa vifo hivyo ni ongezeko kutoka 494 kwa mwaka wa 2012 hadi vifo 556 katika vizazi hai laki moja kwa mwaka huu,hivyo juhudi zaidi zinahitajika ili kupunguza vifo hivyo.

Aidha mradi wa mama na mtoto unaolenga kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto unatekelezwa katika wilaya za Kwimba na Misungwi mkoani Mwanza,ambapo zitatatuliwa changamoto mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hodi za wazazi.


Hata hivyo azma ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kuwa inapunguza vifo vitokanavyo na uzazi ambapo serikali imekuwa ikitumia njia mbalimbali ili kuhakikisha tatizo hilo linapungua,ikiwemo kutoa elimu juu ya umuhimu wa akina mama wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya pamoja na kujenga hodi za akina mama wanaojifungua.
WAMAMA WAJAWAZITO 100 WAMEFARIKI DUNIA MKOANI MWANZA TANGU MWEZI JANUARI HADI AGOSTI MWAKA HUU WAMAMA  WAJAWAZITO  100 WAMEFARIKI  DUNIA  MKOANI  MWANZA  TANGU  MWEZI  JANUARI   HADI  AGOSTI    MWAKA  HUU Reviewed by safina radio on September 20, 2017 Rating: 5

No comments