SUMATRA MKOA WA PWANI KUWAPELEKA MAHAKAMANI MADEREVA WA MAGARI YA ABIRIA AINA KOSTA NA HIECE YASIYOPITA KATIKA KITUO CHA LOLIONDO KIBAHA
TAREHE 27-09-2017
Mamlaka ya
udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA mkoa wa Pwani imesema kuwa
itawapeleka mahakamani pamoja na kuwafungia leseni madereva wa magari ya abiria
aina ya Kosta na hiece asiyopita katika kituo cha Loliondo Kibaha mkoani Pwani.
Hayo
yameelezwa na afisa mfawidhi wa Sumatra mkoa wa Pwani Bw Omary Ayubu katika
zoezi la ukaguzi wa magari aina ya kosta yanayofanya safari zake kati ya Mbezi
na Mlandizi mkoani humo.
Amesema kuwa
mamlaka hiyo haitawafumbia macho madereva wanaokataa kupitia katika kituo cha
loliondo kwa kuwa ndicho kituo cha mabasi madogo na kama kuna malalamiko
yafikishwe katika ofisi za SUMATRA badala ya kugoma na kuwanyima haki ya
kusafiri abiria.
Kwa upande
wake kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Pwani Bw Salim MoriMori
ametoa wito kwa wamiliki wa mabasi kuhakikisha wanaboresha vyombo vyao vya moto
ili kukidhi viwango vya usafirishaji.
Hata hivyo
Bw MoriMori amesema wameamua kufanya operesheni ya kustukiza kwa kushirikiana
na SUMATRA ili kuwajengea madereva kumbukumbu ya kusimamia na kufuata sheria za
usalama barabarani,ambapo katika operesheni hiyo wamefanikiwa kukamata magari
14 ya abiria yaliyokuwa na makosa mbalimbali ikiwemo kika sheria za usalama
barabarani.
SUMATRA MKOA WA PWANI KUWAPELEKA MAHAKAMANI MADEREVA WA MAGARI YA ABIRIA AINA KOSTA NA HIECE YASIYOPITA KATIKA KITUO CHA LOLIONDO KIBAHA
Reviewed by safina radio
on
September 27, 2017
Rating:

No comments