BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LAELEZA WASIWASI WAKE KUHUSU NGUVU ZINAZAZOTUMIWA NA MYANMAR
![]() |
KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA KUSHOTO ANTONIO GUTTERES |
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wake kuhusu nguvu ya kupita kiasi zinazotumiwa na Myanmar wakati wa operesheni yake ya usalama katika jimbo la Rakhine na limetaka hatua za haraka zichukuliwe kukomesha machafuko hayo.
Taarifa ya
pamoja iliyotolewa baada ya kikao cha faragha cha baraza hilo kujadili
machafuko ya Myanmar ambayo yamewalazimu waislamu wa jamii ya Rohingya takriban
laki tatu na themanini kuvuka mpaka na
kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh.
Baraza hilo
la usalama limelaani vikali machafuko hayo na kutoa wito wafanyakazi wa kutoa
misaada ya kibinadamu waruhusiwe kuwafikia watu wanaohitaji msaada katika jimbo
la Rakhine.
Awali katibu
mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa mwito wa operesheni ya kijeshi
katika jimbo hilo ikome mara moja na kudokeza kwamba kuhamishwa kwa lazima kwa
warohingya ni safisha safisha ya kikabila.
BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LAELEZA WASIWASI WAKE KUHUSU NGUVU ZINAZAZOTUMIWA NA MYANMAR
Reviewed by safina radio
on
September 14, 2017
Rating:

No comments