Makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha sekta ya kilimo inatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii na kiuchumi hapa nchini.
TAREHE 6 SEPTEMBA 2017
![]() |
MAKAMU
WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH SAMIA SULUHU HASSANI
|
Makamu wa
rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania amesema kuwa serikali ya awamu ya tano
imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha sekta ya kilimo inatoa mchango mkubwa
katika maendeleo ya jamii na kiuchumi hapa nchini.
Mh Suluhu
ameyasema hayo jijini Dar-es-salaam katika maadhimisho ya miaka 40 ya
ushirikiano kati ya shirika la chakula la umoja wa mataifa FAO na Tanzania,ambapo amesema kuwa moja ya
juhudi hizo za serikali ni kuondoa kodi zote zilizokuwa zikirudisha nyuma
maendeleo ya wakulima nchini.Kwa upande
wake waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi Mh Charles Tizeba amesema kuwa shirika la
chakula duniani limekuwa na mchango mkubwa kwa Tanzania kwa kutoa utaalamu wa
namna ya kukuza sekta ya kilimo hapa nchini.Naye mkurugenzi
mkuu wa shirika hilo Dr Josee Graziano Dasliva amesema kuwa shirika hilo
litaendelea kushirikiana na serikali katika uboreshaji wa sekta ya kilimo na
upatikanaji wa chakula salama kwa wananchi.
Makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha sekta ya kilimo inatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii na kiuchumi hapa nchini.
Reviewed by safina radio
on
September 06, 2017
Rating:

No comments