JESHI LA POLISI MKOANI KAGERA LAKAMATA MAGUNIA 57 YA BANGI
TAREHE 19-09-2017
![]() |
BANGI IKIWA IMEHIFADHIWA KWENYE MAGUNIA |
Jeshi la polisi
mkoani Kagera limefanikiwa kukamata magunia 57 ya bangi yaliyokuwa
yamehifadhiwa katika ghala la mkulima mmoja katika kijiji cha Mtoke toke
wilayani Ngara mkoani humo.
Kwa mujibu
wa kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agostino Olomi amesema kuwa magunia
hayo ya bangi yamekamatwa katika ghala la Bw Saimon Charles baada ya msako
uliofanywa na jeshi la polisi mkoani humo.
Kamanda
Olomi amesema kuwa,baada ya magunia hayo kukamatwa mtuhumiwa amekiri
kujishughulisha na kilimo hicho cha bangi,na atafikishwa mahakamani baada ya
uchunguzi kukamilika.
Hata hivyo
kukamatwa kwa magunia hayo ya bangi kumetokana na operesheni iliyofanywa na
jeshi hilo na kushirikisha vikosi vya polisi vya mikoa ya kagera,Geita na
kigoma.
JESHI LA POLISI MKOANI KAGERA LAKAMATA MAGUNIA 57 YA BANGI
Reviewed by safina radio
on
September 19, 2017
Rating:

No comments