WAOKOAJI HUKO MEXICO WANAJARIBU KUMUOKOA MSICHANA ALIE HAI CHINI YA KIFUSI
TAREHE 21-09-2017
![]() |
WAOKOAJI KATIKA MJI MKUU WA MEXICO, MEXICO CITY |
Waokoaji katika mjini wa Mexico city
wanajaribu kumfikia msichana mdogo, aliye hai chini ya kifusi cha jengo la
shule, lililoporomoka wakati wa Tetemeko la ardhi lililotokea jana.
Waokoaji hao wamekuwa wakimpitishiamtoto
huyo chakula na maji, wakati wakijaribu kutafuta njia ya kuweza kumtoa akiwa
salama kutoka kwenye kifusi hicho.
Hadi sasa watoto wapatao 21 wamekufa
baada ya jengo walilokuwamo kuvunjika, huku wengine wakiwa bado ndani ya kifusi
hicho.
Jumla ya watu zaidi ya mia mbili
wamefariki dunia kutokana na tetemeko hilo.
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto
amesema kila dakika imekuwa ikihesabika katika kuokoa maisha.
Tetemeko hilo la ardhi ni la pili
kuipiga nchi hiyo mwezi huu.
WAOKOAJI HUKO MEXICO WANAJARIBU KUMUOKOA MSICHANA ALIE HAI CHINI YA KIFUSI
Reviewed by safina radio
on
September 21, 2017
Rating:

No comments