KOREA YA KASKAZINI YAFYATUA KOMBORA LA MASAFA MAREFU KUPITIA ANGA YA KISIWA CHA HOKKAIDO NCHINI JAPAN.
TAREHE 15- 09- 2017
![]() |
MOJA YA MAKOMBORA YA KOREA KASKAZINI |
Korea Kaskazini imefyatua kombora la masafa
marefu kupitia anga ya kisiwa cha Hokkaido nchini Japan,ambapo jeshi la Korea Kusini
linasema kuwa kombora hilo limefyatuliwa kutoka maeneo ya karibu na mji mkuu wa
Pyongyang.
Mwandishi wa BBC mjini Tokyo anasema kuwa
kombora hilo lilipita anga za juu zaidi na kwenda mbali zaidi ikilinganishwa na
kombora la awali.
Jaribio hilo linakuja siku chache tu baada
ya baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kuidhinisha vikwazo zaidi dhidi ya
Korea Kaskazini.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa
marekani Rex Tillerson ametoa wito kwa China na Urusi kuchukuwa hatua za moja
kwa moja dhidi ya Pyongyang, huku waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe akitaja
jaribio hilo la hivi punde kuwa ni kitendo cha kuudhi.
Aidha dakika chache baada ya ufyatuzi huo
Korea Kusini ilifyatua makombora mawili ya masafa marefu baharini katika hatua
ya kuionya Korea Kaskazini.
KOREA YA KASKAZINI YAFYATUA KOMBORA LA MASAFA MAREFU KUPITIA ANGA YA KISIWA CHA HOKKAIDO NCHINI JAPAN.
Reviewed by safina radio
on
September 15, 2017
Rating:

No comments