WILAYA YA MONDULI KUBORESHA MAHUSIANO KATI YA KAMBI YA JKT MAKUYUNI NA WANANCHI WANAOZUNGUKA KAMBI HIYO
TAREHE 26-09-2017
![]() |
MKUU WA WILAYA YA MONDULI IDD KIMANTA |
Mkuu wa
wilaya ya Monduli mkoani Arusha Bw Idd Kimanta amesema kuwa,wilaya hiyo itatoa
ushirikiano na kuboresha mahusiano mazuri kati ya kambi ya JKT Makuyuni na
jamii inayozunguka kambi hiyo.
Bw Kimanta
ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kambi ya kikosi namba mia nane thelathini na tisa KJ kilichopo
wilayani Monduli ambapo amesema kuwa ushirikiano kati ya kambi za jeshi na
wananchi unaleta mahusianao mazuri hivyo atashirikiana na viongozi wengine
pamoja na wananchi ili kuhakikisha uhusiano huo unaendelea kuimarika.
Kwa upande
wake mkuu wa jeshi la kujenga taifa JKT Meja Jenerali Michael Issa Moyo
amewataka wakuu wa kambi hiyo kuboresha mafunzo yenye ubunifu yatakayosaidia
kujifunza uzalishaji na kusaidia sera ya uchumi wa viwanda ikiwemo uzalishaji
wa bidhaa mbalimbali.
WILAYA YA MONDULI KUBORESHA MAHUSIANO KATI YA KAMBI YA JKT MAKUYUNI NA WANANCHI WANAOZUNGUKA KAMBI HIYO
Reviewed by safina radio
on
September 26, 2017
Rating:

No comments