Vikosi vya usalama nchini Libya vimetangaza habari ya kupatikana miili 16




Vikosi vya usalama nchini Libya vimetangaza habari ya kupatikana miili 16 ya wahamiaji katika eneo la jangwani, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Misri.
Msemaji wa Jeshi la Taifa la Libya mashariki mwa nchi hiyo  Ahmed al-Mismari, amesema maiti hizo zimepatikana yapata kilomita mia tatu na kumi  kusini magharibi mwa mji wa bandari wa Tobruk.
Afisa huyo wa Jeshi la Libya amesema kwa sasa wanafanya shughuli za kubaini utambulisho wa miili hiyo sanjari na kutafuta miili zaidi katika jangwa hilo.
Haya yanajiri siku chache baada ya kikosi cha gadi ya pwani ya Libya kikiwaokoa wahamiaji zaidi ya 300 katika maji ya magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli.
Mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, wahamiaji 50 wa Kiafrika waliripotiwa kufariki dunia katika jangwa la Sahara huko kaskazini mwa Niger baada ya kutelekezwa na madereva wao.
Hata hivyo  wahamiaji hao haramu hutokea katika nchi za Nigeria, Eritrea, Niger, Somalia, Sudan, Gambia, Senegal, Mali, Morocco na Tunisia. 






Vikosi vya usalama nchini Libya vimetangaza habari ya kupatikana miili 16 Vikosi vya usalama nchini Libya vimetangaza habari ya kupatikana miili 16 Reviewed by safina radio on September 06, 2017 Rating: 5

No comments