SERIKALI KUENDELEA KUPELEKA FEDHA KWENYE SEKTA YA MAJI HAPA NCHINI
TAREHE 21-09-2017
![]() |
WAZIRI MKUU WA TANZANIA MAJALIWA KASSIM MAJALIWA KUSHOTO AKISALIMIANA NA WANANCHI |
Waziri mkuu
wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh majaliwa Kassimu Majaliwa amesema kuwa
serikali itaendelea kupeleka fedha nyingi kwenye sekta ya maji ili kuhakikisha
kuwa tatizo la maji linamalizika hapa nchini.
Mh Majaliwa
ameyasema hayo leo wilayani Longido mkoani Arusha wakati wa sherehe ya uwekaji
wa jiwe la msingi wa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 16 utakaohudumia
wananchi wa wilaya hiyo,ambapo amesema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha
kuwa mwananchi hatembei zaidi ya mita mia nne kupata huduma ya maji.
Amesema kuwa
wilaya ya Longido ina upungufu mkubwa wa maji na hiyo inatokanana jiografia ya
eneo hilo kuwa kame hivyo serikali itaendelea kutenga bajeti kubwa zaidi ili
wananchi wote wa Longido wapate huduma ya maji ambapo kwa mwaka huu serikali imetenga
kiasi cha shilingi bilioni mia sita kwa ajili ya miradi hiyo.
Kwa upande
wake waziri wa maji na umwagiliaji Mh Gerson Lwenge amesema kuwa mradi huo wa
maji utakapokamilika utawanufaisha wananchi wa vijiji vitano vya wilaya hiyo na
maji yake yatatoka katika chanzo cha maji cha mlima Kilimanjaro .
Ameongeza kuwa,wizara yake ina mikakati ya kuhakikisha upatikanaji wa maji unakuwa asilimia 95 kwa mijini na 85 kwa vijijini ufikapo mwaka wa 2025.
SERIKALI KUENDELEA KUPELEKA FEDHA KWENYE SEKTA YA MAJI HAPA NCHINI
Reviewed by safina radio
on
September 21, 2017
Rating:

No comments