WAZIRI WA MAJI, NA UMWAGILIAJI MH. GERSON LWENGE AMEZIAGIZA BODI ZA MABONDE YA MAJI KUWACHUKULIA HATUA WATU WANAOFANYA KAZI KARIBU NA VYANZO VYA MAJI

TAREHE 29-09-2017
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI  MH.GERSON  LWENGE
Waziri wa maji na umwagiliaji Mh Gerson Lwenge ameziagiza bodi za mabonde ya maji nchini kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya watu wanaofanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji ili kudhibiti tatizo la upotevu wa maji.

Mh Lwenge ametoa maagizo hayo wakati akizindua bodi mpya ya bonde la ziwa Tanganyika mkoani Kigoma pamoja na ofisi mpya za mamlaka ya bonde hilo,ambapo amesema kuwa rasilimali za maji ni lazima zisimamiwe na bodi ili kuzua watu wanaofanya shughuli zao kandokando ya vyanzo hivyo na kusababisha upungufu wa maji kwa wananchi.

Amesema kuwa bodi za maji zinazoanzishwa na serikali ni muhimu sana,na lazima wajue wajibu wao kwani kuna baadhi ya wajumbe wanaoteuliwa wakifikiri ni kwenda kupata posho pekee bila kujua kuwa wanatakiwa kwenda kushughulikia kero za wananchi ili kuhakikisha wanapata maji safi na salama.

Aidha waziri huyo ameongeza kuwa,hatasita kumfukuza mwenyekiti wa bodi ya maji yeyote hapa nchini atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwemo kupeleka taarifa sahihi kwa waziri wa maji kama sheria inavyoelekeza.


Hata hivyo ziwa la bonde Tanganyika limeelezewa kupungua kina chake cha maji kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na shughuli za kibinadamu zinazofanywa na baadhi ya watu karibu na vyanzo vya maji.
WAZIRI WA MAJI, NA UMWAGILIAJI MH. GERSON LWENGE AMEZIAGIZA BODI ZA MABONDE YA MAJI KUWACHUKULIA HATUA WATU WANAOFANYA KAZI KARIBU NA VYANZO VYA MAJI WAZIRI   WA  MAJI, NA  UMWAGILIAJI  MH. GERSON  LWENGE  AMEZIAGIZA  BODI ZA MABONDE  YA   MAJI  KUWACHUKULIA  HATUA  WATU  WANAOFANYA  KAZI KARIBU  NA   VYANZO  VYA  MAJI Reviewed by safina radio on September 29, 2017 Rating: 5

No comments