MKUU WA MKOA WA ARUSHA BW. MRISHO GAMBO AMECHANGIA SHILINGI MILIONI MOJA NA MIFUKO HAMSINI YA SARUJI KWA AJILI YA UJENZI WA CHUMBA CHA UPASUAJI KATIKA ZAHANATI YA OLDONYOWAS MKOANI ILIYOPO ARUSHA
TAREHE 15-09-2017
![]() |
MKUU WA MKOA WA ARUSHA BW. MRISHO GAMBO |
Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Mrisho Gambo amechangia kiasi cha shilingi
milioni moja pamoja na mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya kujenga chumba cha
upasuaji katika zahanati ya Oldonyowas iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya
Arusha.
Gambo amechangia fedha hizo alipokuwa akijibu kero za
wananchi wa kata hiyo za kuiomba serikali iwajengee chumba cha upasuaji
kufuatia akina mama na watoto kufariki dunia pindi wanapoenda kujifungua.
Amesema kuwa kutokana na akina mama kukabiliwa na changamoto ya
chumba cha upasuaji atatoa kiasi hicho cha milioni moja pamoja na mifuko 50 ili
kuwezesha kunusuru maisha ya wamama wajawazito pindi wanapotaka kujifungua.
Kufuatia changamoto hiyo mkuu huyo wa mkoa amekubaliana na wananchi wa Oldonyoas pamoja na Oldonyosambu
kuchanga kila mmoja kiasi cha shilingi elfu 30 ili kuweza kujenga chumba hicho
na baadaye halmashauri itamalizia ujenzi huo ambapo itakapomalizika zahanati
hiyo itapanda hadhi na kuwa kituo cha afya.
Awali wakieleza kero zao kwa mkuu wa mkoa wananchi hao wamesema
kuwa katika kata hiyo wanakabiliwa na changamoto ya wamama na watoto
kupoteza maisha mara wanapofika katika zahanati hiyo kujifungua kutokana na ukosefu
wa chumba cha upasuaji.
Walitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na tatizo la
maji,kutokuwepo kwa kituo cha polisi pamoja na mahakama na hivyo kuiomba
serikali kuwasaidia kutatua changamoto hizo.
MKUU WA MKOA WA ARUSHA BW. MRISHO GAMBO AMECHANGIA SHILINGI MILIONI MOJA NA MIFUKO HAMSINI YA SARUJI KWA AJILI YA UJENZI WA CHUMBA CHA UPASUAJI KATIKA ZAHANATI YA OLDONYOWAS MKOANI ILIYOPO ARUSHA
Reviewed by safina radio
on
September 15, 2017
Rating:

No comments