WANASAYANSI WATAKIWA KUWASAIDIA WAKULIMA WA KILIMO CHA MITI HAPA NCHINI.

TAREHE 29-09-2017

WAZIRI  WA MALI ASILI NA UTALII PRO. JUMANNE  MAGHEMBE
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe amewataka Wanasayansi na Mashirika yanayuojishughulisha na uhifadhi wa misitu ya ndani na nje kuwasaidia wakulima wa kilimo cha miti kubuni mbinu mbadala wakati wakisubiri kuvuna miti yao.

Prof. Maghembe ameeleza hayo Mkoani Morogoro katika kikao cha uimarishaji misitu na mazao ya misitu kinachojadili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa,Dkt. Kebwe Stivin Kebwe ametoa wito kwa jamii kutunza Mzingira na Hifadhi za taifa ili kujiepusha na madhara ya ukame na majangwa yanayoweza kutokea.


Kikao hicho kimeandaliwa kwa pamoja na Muungano wa Vikundi vya Wakulima (MVIWATA) na We Effect ya nchini Kenya na kushirikiana na mataifa kumi na saba (17)
WANASAYANSI WATAKIWA KUWASAIDIA WAKULIMA WA KILIMO CHA MITI HAPA NCHINI. WANASAYANSI  WATAKIWA   KUWASAIDIA   WAKULIMA   WA  KILIMO  CHA  MITI  HAPA  NCHINI. Reviewed by safina radio on September 29, 2017 Rating: 5

No comments