MAMIA YA VIJANA WAANDAMANA KATIKA MAENEO YA UCHIMBAJI WA MADINI NCHINI GUINEA.
TAREHE 22-09-2017
![]() |
VIJANA WAKIANDAMANA NCHINI GUINEA |
Mamia ya vijana wamefanya maandamano katika maeneo ya uchimbaji wa madini nchini Guinea, huku wakichoma moto kituo cha polisi pamoja na jengo lingine la umma.
Habari kutoka mji wa Kolaboui, katika wilaya ya Boke, zinasema kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa katika makabiliano hayo kati ya walinda usalama na waandamanaji waliokuwa na marungu.
Wakaazi wa eneo hilo wanadai kutonufaika na utajiri wa madini ulio katika eneo lao.
Madini hayo ya Bauxite (Bazait) hutumika kuzalishia Alumini.
MAMIA YA VIJANA WAANDAMANA KATIKA MAENEO YA UCHIMBAJI WA MADINI NCHINI GUINEA.
Reviewed by safina radio
on
September 22, 2017
Rating:

No comments