RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP AMETANGAZA PUNGUZO KUBWA LA KODI
TAREHE 28-09-2017
![]() |
RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP |
Trump ametangaza kupunguza kodi kwenye biashara na amesisitiza kuwa ataondoa kodi ya urithi.
Amesema kuwa wafanyakazi wanawake kwa wanaume ndiyo watakao nufaika na hatua hiyo na si wale wenye mapato makubwa na kudai kuwa mfumo wao mpya unalenga kuleta mabadiliko ambayo yatamlinda mtu wa kipato cha chini, cha kati na katika ngazi ya kaya na siyo kwa matajiri.
Hatua hii ni kutekeleza mapendekezo ya chama chake cha Republicans, huku Democrats wakiwa na maoni tofauti kwamba mabadiliko hayo yataziumiza familia zenye kipato cha kati na kupunguza kipato chao hasa wajane na watoto.
RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP AMETANGAZA PUNGUZO KUBWA LA KODI
Reviewed by safina radio
on
September 28, 2017
Rating:

No comments