ASKARI WATATU WA ISRAEL WAMEUAWA
TAREHE 26-09-2017
Taarifa za
polisi wa Israel zinasema, askari watatu wa nchi hiyo wameuwawa katika maeneo
ya Ukingo wa Magharibi,ambapo mauaji hayo yametokea baada ya Mpalestina mmoja
kuwafyatulia askari hao risasi.
Mtu huyo pia
alimjeruhi mmoja wa askari hao wa Israel kabla ya yeye mwenyewe kuuwawa kwa
kupigwa risasi na Mashambulio hayo
yametokea wakati ambapo mjumbe wa Marekani Jason Greenblatt alikuwa mjini
Jerusalem kwa mazungumzo yaliyolenga kufufua upya mpango wa amani ya Mashariki
ya Kati.
Kwa mujibu wa
taarifa Mpalestina huyo alifika katika lango la Har Adar pamoja na Wapalestina
wengine ambao hufanya kazi za vibarua na mara moja alitoa silaha yake na
kuwalenga maafisa wa polisi.
Hata
hivyo Har Adat ni makaazi yaliyopo kaskazini magharibi Jerusalem karibu na
Msitari wa Kijani unaotenganisha Ukanda wa Gaza na Israel.
ASKARI WATATU WA ISRAEL WAMEUAWA
Reviewed by safina radio
on
September 26, 2017
Rating:

No comments