Raia huyo wa Brazil pamoja na mwenzake wa Uruguay walilazimika kutawanywa katika chumba cha maandalizi kufuatia majibizano makali ya mechi ya siku ya Jumapili ambapo klabu hiyo iliibuka mshindi dhidi ya Lyon.
Na sasa kulingana na gazeti
la Spanish Outlet Sport, mchezaji ghali zaidi duniani amemtaka mwenyekiti wa
klabu hiyo Nasser Al-Khalifi kumuuza mwenzake akisema kuwa uhusiano wake na Cavani
umeharibika na hivyobasi hawawezi kucheza pamoja.
Inaaminika kwamba Neymar
anataka mshambuliaji huyo kuuzwa wakati wa kufunguliwa kwa dirisha la uhamisho
mwezi Januari.
Tatizo lilitokea kunako
dakika ya 79 wakati ambapo Kylian Mbappe alikuwa amejishindia penalti baada ya
kufanyiwa madhambi ndani ya eneo hatari.
Neymar alitaka kuipiga
penalti hiyo badala ya mpiga penalti wa kila mara Edison Cavani.
Raia huyo wa Uruguay ambaye
hapo awali alikuwa amehusika katika mgogoro na mchezaji mwengine wa Brazil Dani
Alvez kuhusu kupiga mkwaju wa adhabu kabla ya raia huyo wa Brazil kumpatia
mpira huo Neymar, alikataa katakata kabla ya kupiga penalti hiyo ambayo iliokolewa.
Cavani baadaye alimuandama
Neymar baada ya mechi kabla ya wachezaji wenza Thiago Motta na Marquinhos
kuingilia kati na kuwatawanya.

No comments