WIZARA YA MAMBO YA NJE YA MAREKANI KUTATHIMINI IWAPO ITAFUNGA UBALOZI WAKE NCHINI CUBA









TAREHE 18-09-2017
WAZIRI  WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI REX TILLERSON
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema Washington inatathmini iwapo ifunge ubalozi wake nchini Cuba, baada ya kutokea mlolongo wa mashambulizi ya kelele kwa wafanyakazi wake.
Kwa sasa zaidi ya wafanyakazi 20 wa ubalozi wa Marekani wameripotiwa kuwa na matatizo ya kupoteza uwezo wa kusikia au kupatwa na mfadhaiko kutokana na sauti hiyo.
Marekani imeiambia Cuba kuwa ina jukumu la kuwalinda wafanyakazi wote wakigeni wakiwemo Wamarekani.

Cuba imekana kuhusika na suala hilo huku uchunguzi zaidi ukiendelea ,kujua chanzo cha watu hao kukumbwa na matatizo hayo ya kiafya wanayoyazungumzia.
WIZARA YA MAMBO YA NJE YA MAREKANI KUTATHIMINI IWAPO ITAFUNGA UBALOZI WAKE NCHINI CUBA WIZARA  YA  MAMBO  YA  NJE   YA  MAREKANI  KUTATHIMINI  IWAPO  ITAFUNGA  UBALOZI  WAKE  NCHINI    CUBA Reviewed by safina radio on September 18, 2017 Rating: 5

No comments