MKUU WA MKOA WA ARUSHA BW. MRISHO GAMBO AMELIAGIZA SHIRIKA LA UMEME TANESCO KUWAPATIA UMEME WANANCHI WA MALULA WILAYANI ARUMERU MKOANI ARUSHA
TAREHE 29-09-2017
![]() |
MKUU WA MKOA WA ARUSHA BW. MRISHO GAMBO |
Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Mrisho Gambo ameliagiza
shirika la umeme Tanzania TANESCO kuwapatia huduma ya umeme wananchi wa Malula
na mji mdogo wa Usa river katika wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Agizo hilo la mkuu wa mkoa ni utekelezaji wa agizo
las rais Mh John Magufuli alilolitoa wakati akiwa njiani kuelekea uwanja wa
ndege wa kimataifa wa KIA mara baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani Arusha.
Kwa upande Mwakulishi wa meneja wa umeme hapa nchini
mkoa wa Arusha Mhandisi Joanisiano Shamba amesema kuwa wananch hao watapata
umeme kupitia mradi wa wakala wa nishati ya umeme vijijini REA awamu ya tatu .
Hata hivyo akiwa mkoani
Arusha rais Magufuli alisimamishwa na wananchi kwa lengo la kumwelezea kero
mbalimbali zinazowakabili ikiwemo tatizo la umeme,ambapo aliwataka wananchi
kushirikiana na serikali ili waweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
MKUU WA MKOA WA ARUSHA BW. MRISHO GAMBO AMELIAGIZA SHIRIKA LA UMEME TANESCO KUWAPATIA UMEME WANANCHI WA MALULA WILAYANI ARUMERU MKOANI ARUSHA
Reviewed by safina radio
on
September 29, 2017
Rating:

No comments