MADEREVA 64 WA MAGARI YA ABIRIA KUTOKA MIKOA MITATU YA KANDA YA KASKAZINI WAFUNGIWA LESENI ZAO.
TAREHE 19-09-2017
![]() |
MADEREVA |
Jumla ya
madereva 64 wa magari ya abiria kutoka mikoa mitatu ya kanda ya kaskazini
wamefungiwa leseni zao kwa kipindi cha miezi sita baada ya kukutwa na makosa
mbalimbali ya uvunjifu wa sheria za usalama barabarani.
Adhabu hiyo
imetolewa na kamanda wa kikosi cha usalama wa barabarani hapa nchini SACP
Fortunatus Musilimu wakati wa operesheni maalumu aliyoifanya ya kubaini
madereva wanaokiuka sheria za usalama wa barabarani katika mikoa ya
Arusha,Kilimanjaro na Manyara.
Kamanda Musilimu
amesema kuwa kati ya madereva hao 47 ni kutoka mkoa wa Kilimanjaro,13 kutoka
mkoa wa Arusha na 4 wa mkoa wa Manyara ambao watatumikia adhabu hiyo kw
akipindi cha miezi na baada ya muda huo kwisha madereva hao watatainiwa upya ili
kuona kama wanafaa kurudishiwa leseni zao.
Amesema kuwa
moja ya makosa hayo ni kuendesha kwa mwendo kasi hali inayohatarisha maisha ya
abiria,ambapo amesema kuwa operesheni hiyo itakuwa endelevu lengo likiwa ni
kupunguza ajali zitokanazo na uzembe na kupoteza nguvu kazi ya taifa.
MADEREVA 64 WA MAGARI YA ABIRIA KUTOKA MIKOA MITATU YA KANDA YA KASKAZINI WAFUNGIWA LESENI ZAO.
Reviewed by safina radio
on
September 19, 2017
Rating:

No comments