Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu amewataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya hapa nchini kuwachukulia hatua za kisheria watu wote wanaouza madawa ya tiba asili kinyume na sheria.

                                          TAREHE 6 SEPTEMBER 2017
WAZIRI WA AFYA WAZEE JINSIA NA WATOTO MH UMMY MWALIMU

Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu amewataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya hapa nchini kuwachukulia hatua za kisheria  watu wote wanaouza madawa ya tiba asili kinyume na sheria.
Mh Mwalimu ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Konde Mh Khatibu Haji aliyetaka kujua ni  utaratibu gani unaotumiwa na serikali katika kuwaruhusu watu mbalimbali kuuza madawa ya tiba asili kutokana na matangazo mengi yanayobandikwa mitaani na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.
Amesema kuwa ili mtu aruhusiwe kuuza madawa ya tiba asili ni lazima asajiliwe kwenye baraza la tiba asili na tiba mbadala baada ya kudhibitishwa na mkemia mkuu wa serikali pamoja na mamlaka ya chakula na dawa TFDA kama hazina madhara kwa binadamu hivyo mtu yeyote anayefanya biashara hiyo bila kusajiliwa anavunja sheria hivyo anatakiwa kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Mh waziri amesema utaratibu wa usajili upo kwa mujibu wa sheria ya nchi ya mwaka wa 2002 na kanuni zake,ambapo pia amewataka wananchi kufanya mazoezi ili kuepukana na matatizo mbalimbali yanayowafanya kukimbilia kununua dawa hizo ikiwemo upungufu wa nguvu za kiume.

Hata hivyo bunge la kumi na moja mkutano wa nane unaendelea mjini Dodoma ambapo wabunge watajadili miswada mbalimbali ya kisheria na mkutano huo unatarajiwa kuhitimishwa Sept 15 mwaka huu.
Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu amewataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya hapa nchini kuwachukulia hatua za kisheria watu wote wanaouza madawa ya tiba asili kinyume na sheria. Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu amewataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya hapa nchini kuwachukulia hatua za kisheria  watu wote wanaouza madawa ya tiba asili kinyume na sheria. Reviewed by safina radio on September 06, 2017 Rating: 5

No comments