Rais wa Urusi Vladimir Putin amelaani vitendo vya Korea Kaskazini vya kufanya majaribio ya mpango wake wa kinyuklia




Rais wa Urusi Vladimir

Rais wa Urusi Vladimir Putin amelaani vitendo vya Korea Kaskazini vya kufanya majaribio ya mpango wake wa kinyuklia na kurusha makombora na kuongeza kua  nchi zingine zenye nguvu duniani zinapaswa kujizuia kuuchochea  zaidi mzozo wa Korea Kaskazini ambao unaweza kusababisha janga kubwa duniani.
Katika mkutano na wanahabari hapo jana, Putin amesema anabashiri kutokea janga iwapo njia nyingine isipokuwa ya kidiplomasia itatumika kukabiliana na Korea Kaskazini akihimiza mazungumzo ya amani badala kutumia nguvu za kijeshi ambazo huenda zikasababisha athari kubwa ulimwenguni.
Rais huyo wa Urusi amesema  kuiongezea Korea Kaskazini vikwazo ni kupoteza wakati, kwani Wakorea Kaskazini wako radhi hata kula nyasi kuliko kuachana na mpango wake wa kinyuklia.

Marekani imeishutumu Korea Kaskazini kwa kufanya kila njia kuingia vitani,ambapo nchi hiyo ilifanya jaribio kubwa la bomu la haidrojen siku ya Jumapili ambalo limelaaniwa vikali na jumuiya ya kimataifa.
Rais wa Urusi Vladimir Putin amelaani vitendo vya Korea Kaskazini vya kufanya majaribio ya mpango wake wa kinyuklia Rais wa Urusi Vladimir Putin amelaani vitendo vya Korea Kaskazini vya kufanya majaribio ya mpango wake wa kinyuklia Reviewed by safina radio on September 06, 2017 Rating: 5

No comments