WAZIRI WA UJENZI NA MAWASILIANO MH. MAKAME MBARAWA MNYAA AWATAKA WADAU WA MAWASILIANO YA ANGA KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA SEKTA HIYO.
TAREHE 20-09-2017
![]() |
WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO MH. MAKAME MBARAWA MNYAA |
Waziri wa
ujenzi uchukuzi na mawasiliano Mh Makame Mbarawa Mnyaa amewataka wadau wa
mawasiliano ya anga hapa nchini kutatua changamoto zilizopo katika sekta hiyo
ili kuwezesha uchumi wa Tanzania ya viwanda.
Mh Mnyaa
ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika kongamano la kwanza la mamlaka ya
usafiri wa anga jijini Dar-es-salaam,ambapo amesema kuwa serikali iko tayari
kushirikiana na wadau wa mamlaka ya anga katika kukabiliana na changamoto
zinazokabili mamlaka hiyo ikiwemo upungufu wa wataalamu.
Amesema kuwa
serikali imeamua kukutana na wadau hao ili kujadiliana namna ya kumaliza
changamoto hizo zinazoikabili sekta ya anga ikiwemo usafirishaji wa bidhaa
mbalimbali kupitia viwanja vya ndege vya nje badala ya viwanja vya ndani hali
inayosababisha Tanzania kupoteza mapato mengi ambayo yangeweza kuinua uchumi wa
Taifa.
Kwa upande
wake mkurungenzi mkuu wa mamlaka ya usafiri wa anga nchini TCAA Bw Hamza Johari
amewataka wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ili Tanzania iweze kuwa na
wataalamu wenngi zaidi hasa katika sekta ya anga ambayo ina upungufu mkubwa wa
wataalamu.
Hata hivyo
mamlaka ya anga hapa nchini ina wataalamu 20 pekee huku mahitaji halisi ya
wataalamu wanaotakiwa ikiwa ni 50.
WAZIRI WA UJENZI NA MAWASILIANO MH. MAKAME MBARAWA MNYAA AWATAKA WADAU WA MAWASILIANO YA ANGA KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA SEKTA HIYO.
Reviewed by safina radio
on
September 20, 2017
Rating:

No comments