MAMLAKA ZA UPIMAJI MAENEO MKOANI DODOMA ZIMEAGIZWA KUTOA VIWANJA KWA GHARAMA NAFUU
TAREHE 28-09-2017
Mamlaka zinazohusika na upimaji wa maeneo mkoani Dodoma zimeagizwa kuzipatia viwanja
kwa gharama nafuu taasisi zinazotaka kujenga ofisi na makazi mkoani humo ili kuunga
mkono mpango wa serikali wa kuhamia Dodoma.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Bw
Jordan Rwigimbana wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi
mbalimbali ya ujenzi inayoendelea mkoani humo.
Katika ziara hiyo mkuu huyo wa mkoa amepokea
malalamiko kutoka kwa baadhi ya taasisi za kukwamisha ujenzi na kutotoa ushirikiano
hali iliyomlazimu kuzitaka mamlaka husika kuzipatia taasisi hizo maeneo kwa
gharama nafuu ili nyumba zinazojengwa zikamilike kwa wakati.
Hata hivyo mji wa Dodoma unaendelea kujengwa baada
ya serikali ya awamu ya tano kuamua kuhamishia shughuli zake mkoani humo ambako
ndiko makao makuu ya nchi.
MAMLAKA ZA UPIMAJI MAENEO MKOANI DODOMA ZIMEAGIZWA KUTOA VIWANJA KWA GHARAMA NAFUU
Reviewed by safina radio
on
September 28, 2017
Rating:

No comments