SANCHEZ AINGOZA ARSENAL KATIKA USHINDI WA 3-1 DHIDI YA FC COLOGNE YA UJERUMANI KATIKA MICHUANO YA EUROPA LIGI







TAREHE 15-09-2017


MCHEZAJI WA ARSENAL ALEXIS  SANCHEZ



Alexis Sanchez aliisaidia Arsenal kutoka nyuma na kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya klabu ya Ujerumani Cologne katika mechi ya Yuropa iliocheleweshwa kwa saa moja kutokana na matatizo ya mashabiki.
Sanchez ambaye karibia aihame klabu hiyo ili kujiiunga na Manchester City katika siku ya mwisho ya uhamisho , aliuchukua mpira nje ya eneo hatari na kuupinda huku kipa Timo akishindwa kuokoa mkwaju huo.
Mechi hiyo hatahivyo haikuanza katika muda iliopangiwa baada ya maelfu ya mashabiki wa Cologne kuwasili katika uwanja wa Emirates bila tiketi na baadaye kuzozana na wanaowakaribisha wageni ndani ya uwanja huo.
Na mechi ilipoanza , Cologne ilichukua uongozi baada ya Jhon Cordoba kumfunga kipa David Ospina akiwa maguu 40.

Mshambuliaji Olivier Giroud alipiga nje kichwa cha wazi akiwa maguu sita pekee karibu na goli .
Lakini mchezaji wa ziada Sead Kolasinac alisawazisha kabla ya Sanchez kufunga bao la pili.
Beki wa kulia wa Arsenal Hector baadaye alifunga bao la tatu huku kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere akiichezea klabu hiyo kwa mara ya kwanza tangu Agosti 2016.

Katika mchezo mwingine Everton wameanza vibaya michuano ya Europa baada ya kufungwa bao 3 kwa nunge na Atlanta, huku Villareal wakiipiga Fc Astana bao 3 kwa 1.

Andre Silva aliifungia Ac Millan hattrick wakati wakiichapa Austria Vienna bao 5 kwa 1, huku Suso na Calhanoglu wakiipatia Ac Millan mabao mengine na lile la Austria Vienna likiwekwa kimiani na Borkavic.
SANCHEZ AINGOZA ARSENAL KATIKA USHINDI WA 3-1 DHIDI YA FC COLOGNE YA UJERUMANI KATIKA MICHUANO YA EUROPA LIGI SANCHEZ AINGOZA ARSENAL KATIKA USHINDI  WA 3-1 DHIDI  YA  FC  COLOGNE YA  UJERUMANI  KATIKA  MICHUANO YA  EUROPA  LIGI Reviewed by safina radio on September 15, 2017 Rating: 5

No comments