MKUTANO WA SABA WA BARAZA LA WAWAKILISHI KUANZA KESHO JUMATANO
TAREHE 26-092017
![]() |
Mkutano wa
saba wa baraza la tisa la wawakilishi unatarajiwa kuanza Jumatanao wiki hii
ambapo patakuwepo na shughuli mabalimbali ikiwemo kipindi cha maswali na majibu
ambapo jumla ya maswali mia moja thelethini na saba yatajibiwa.
Akitoa
taarifa ya kuanza kwa mkutano huo mbele ya waandishi wa habari mjini Unguja
katibu wa baraza la wawakilishi Raya Issa amesema kuw apamoja na mambo mengine
muswada ya sheria ambayo iliwasilishwa na kusomwa katika mkutano uliopita
itasomwa na kujadiliwa tena katika vikao hivyo vya wawakilishi.
Katibu huyo
ametaja miswada itakayojadiliwa kuwa ni pamoja na mswada wa kufuta sheria namba
tatu ya mahakama ya kadhi ya mwaka wa 1985 na mswada wa sheria ya kuanzisha
baraza la taifa la biashara.
Hata hivyo
mkutano huo pia unatarajia kujadili ripoti za wizara za serikali ya mapinduzi
ya Zanzibar kuhusu utekelezaji wa maagizo ya kamati za baraza hilo ikiwemo ripoti
ya utekelezaji wa mamlaka ya maji Zanzibar ZAWA.
MKUTANO WA SABA WA BARAZA LA WAWAKILISHI KUANZA KESHO JUMATANO
Reviewed by safina radio
on
September 26, 2017
Rating:

No comments