WATU ZAIDI YA 140 WAFARIKI DUNIA KATIKA TETEMEKO LA ARDHI NCHINI MEXICO





TAREHE 20-09 -2017
MIILI  YA  WATU  WALIOFARIKI DUNIA
Tetemekokubwa la ardhi limekumba maeneo ya katikati mwa Mexico na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 140 huku jitihada za uokozi zikiendelea.

Tetemeko lenye nguvu ya kipimo cha saba nukta moja kwa vipimo vya Richter limedondosha karibu majengo 30 katika mji mkuu wa Mexico city.

Watu wanaotoa huduma za dharura wakisaidiwa na mamia ya watu wanaojitolea bado wanaendelea kutafuta manusura ambao wamefukiwa na kifusi.

Maafisa wa serikali nchini wanasema idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka ambapo mwandishi wa habari aliyekuwa mjini Mexco city Bi Natasha Pizzey amesema kuwa kuna idadi kubwa ya watu waliofukiwa na kifusi baada ya majengo kuporomoka.


Mapema mwezi huu tetemeko hilo la ardhi pia lilipita katika eneo la pwani ya kusini magharibi mwa Mexico na kusababisha vifo vya watu 90.
WATU ZAIDI YA 140 WAFARIKI DUNIA KATIKA TETEMEKO LA ARDHI NCHINI MEXICO WATU  ZAIDI  YA   140  WAFARIKI   DUNIA    KATIKA  TETEMEKO  LA ARDHI   NCHINI  MEXICO Reviewed by safina radio on September 20, 2017 Rating: 5

No comments