SERIKALI KUTOA NAKALA ZA RIPOTI KWA MAANDISHI YA NUKTA NUNDU ILI KUWASAIDIA WATU WENYE ULEMAVU WA KUTOONA.
TAREHE 22-09-2017
![]() |
CAG PROFESSA MUSSA ASSAD |
Mkaguzi na mdhibiti
mkuu wa hesabu za serikali CAG Professa Mussa Assad amesema kuwa ofisi yake iko
kwenye mchakato wa kutoa nakala za ripoti zake kwa maandishi ya nukta nundu ili
kuwasaidia watu wenye ulemavu wa kutoona.
Professa Assad
ameyasema hayo wakati akifungua warsha kuhusu namna ya kusambaza na kukusanya
maoni ya toleo maalumu kwa mwaka wa fedha wa 2015-2016 mjini Moshi,ambapo
amesema kuwa ripoti hizo zitaanza kutolewa kwa maandishi katika mwaka ujao wa
fedha.
Amesema kuwa
kituo cha usambazaji na ukusanyaji wa maoni ya toleo maalumu za mdhibiti na
mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ni cha nne na kimeshirikisha asasi za kiraia
kutoka mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Manyara na Tanga.
SERIKALI KUTOA NAKALA ZA RIPOTI KWA MAANDISHI YA NUKTA NUNDU ILI KUWASAIDIA WATU WENYE ULEMAVU WA KUTOONA.
Reviewed by safina radio
on
September 22, 2017
Rating:

No comments