KANSELA WA UJERUMANI, ANGEL MERKEL AMESEMA KUWA CHAMA CHAKE HAKITAEGEMEA SERA ZA MRENGO WA KULIA.

TAREHE 26-09-2017

ANGELA  MERKEL
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema kuwa chama chake hakitaegemea sera za mrengo wa kulia kujaribu kuwashawishi wapiga kura ambao walimuacha wakati alipokuwa anapambana na chama kinachopinga sera za uhamiaji cha AfD wakati wa uchaguzi wa jumapili.

Merkel amesema atajaribu kadiri awezavyo kurejesha Imani ya idadi kubwa ya watu ambayo walijisikia kutengwa.

Mafanikio ya chama cha mrengo wa kushoto cha AfD Kimekiacha chama chake Merkel,CDC bila kuwa na mshirika wa wazi kuunda serikali.


Merkel amesema alitaka kuunda serikali imara ambapo amezungumza na chama cha Liberals na Greens pamoja na Social Democrats ambao walijitoa kuungana kwa mara nyingine na Christian Democrats.
KANSELA WA UJERUMANI, ANGEL MERKEL AMESEMA KUWA CHAMA CHAKE HAKITAEGEMEA SERA ZA MRENGO WA KULIA. KANSELA   WA  UJERUMANI,   ANGEL   MERKEL  AMESEMA   KUWA  CHAMA   CHAKE  HAKITAEGEMEA  SERA   ZA  MRENGO    WA  KULIA. Reviewed by safina radio on September 26, 2017 Rating: 5

No comments