NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MH. MERNAD KALEMANI AMELIAGIZA JESHI LA POLISI MKOANI SINGIDA KUMKAMATA MENEJA WA SHIRIKA LA UMEME TANZANIA TANESCO WA MJI WA ITIGI .


14-09-2017
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KUSHOTO MH. MERNAD KALEMANI.


Naibu waziri wa nishati na madini Mh Mernad Kalemani ameliagiza jeshi la polisi mkoani Singida kumtafuta na kumkamata meneja wa shirika la umeme Tanzania Tanesco wa mji wa Itigi anayetuhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa wananchi wa mji huo.

Mh Kalemani ametoa maagizo hayo wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Itigi mkoani Singida,ambapo amesema kuwa meneja huyo ambaye ni Bw Ramadhan Rajabu alijipatia kiasi cha shilingi milioni 60 baada ya kuwarubuni wananchi kwamba atawaunganishia umeme na kuwapa risiti bandia.

Aidha kutokana na udanganyifu huo naibu waziri huyo amelitaka shirika la umeme kuwaunganishia huduma ya umeme wananchi mia tano wa mji huo waliokatiwa umeme baada ya kukutwa na risiti bandia na ambao wamejiunganishia huduma ya umeme kinyemela baada ya kubainika kuwa hawana hatia.


Hata hivyo Dr Kalemani alikuwa mkoani Singida katika mji wa Itigi kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.Naibu waziri wa nishati na madini Mh Mernad Kalemani ameliagiza jeshi la polisi mkoani Singida kumtafuta na kumkamata meneja wa shirika la umeme Tanzania Tanesco wa mji wa Itigi anayetuhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa wananchi wa mji huo.


NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MH. MERNAD KALEMANI AMELIAGIZA JESHI LA POLISI MKOANI SINGIDA KUMKAMATA MENEJA WA SHIRIKA LA UMEME TANZANIA TANESCO WA MJI WA ITIGI . NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MH. MERNAD KALEMANI AMELIAGIZA JESHI LA POLISI MKOANI SINGIDA KUMKAMATA MENEJA WA SHIRIKA LA UMEME TANZANIA TANESCO WA MJI WA ITIGI . Reviewed by safina radio on September 14, 2017 Rating: 5

No comments