MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA ARUSHA MH. AMINA MOLLEL AIOMBA SERIKALI KUIPATIA MAJI SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI

TAREHE  18-09-2017


MBUNGE  WA  VITI MAALUM  MKOA  WA ARUSHA  MH. AMINA MOLLEL



Mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha Mh Amina Mollel ameiomba serikali kuipatia maji shule ya sekondari Mlangarini  kwani kwa sasa inakabiliwa na changamoto hiyo hali ambayo inaweza kuleta madhara kwa wanafunzi.

Mh Amina Mollel ametoa maombi hayo mbele ya mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Mrisho Gambo mara baada ya kufanya ziara shuleni hapo kwa lengo la kubaini changamoto zinazoikabili shule hiyo.

Amefafanua kuwa kutokana na tatizo hilo wanafunzi wa shule hiyo hulazimika kufuata maji mtoni na kuhatarisha maisha ya wanafunzi  hao hasa wa kike ambao hunusirika kubakwa hivyo shule hiyo inatakiwa kupatiwa mradi wa maji haraka iwezekanavyo ili kusogeza huduma karibu na wanafunzi.

Akijibu kero hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha mkurugenzi wa halmashuri ya wilaya ya Arusha Dk Wilson Mahera amesema kuwa changamoto hiyo itatatuliwa mapema iwezekanavyo kwani tayari upo mradi wa benki ya dunia unaopita maeneo hayo hivyo wanafunzi hao hawatakiwi kuwa na wasiwasi.

MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA ARUSHA MH. AMINA MOLLEL AIOMBA SERIKALI KUIPATIA MAJI SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI MBUNGE   WA  VITI  MAALUM  MKOA  WA  ARUSHA  MH.  AMINA  MOLLEL  AIOMBA  SERIKALI  KUIPATIA  MAJI   SHULE   YA    SEKONDARI   MLANGARINI Reviewed by safina radio on September 18, 2017 Rating: 5

No comments