WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. MAJALIWA KASSIMU MAJALIWA AMESEMA SERIKALI ITAENDELEA KUPELEKA FEDHA KWENYE MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO.
TAREHE 15-09-2017
![]() |
WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. MAJALIWA KASSIMU MAJALIWA |
Waziri mkuu
wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassimu Majaliwa amesema kuwa serikali itaendelea kupelekeka fedha kwenye miradi mbalimbali ya
maendeleo hapa nchini ikiwemo sekta ya afya.
Mh Majaliwa
ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hotuba ya kuharisha
mkutano wa nane wa bunge ulioanza Septemba 05 mwaka huu,ambapo amesema kuwa nia
ya serikali kupeleka fedha hizo ni ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa maeneo mbalimbali
hapa nchini.
Amesema kuwa
katika sekta ya afya kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 upatikanaji wa dawa katika
bohari ya dawa nchini MSD umeongezeka hadi kufikia asilimia 82 ikilinganishwa
na wastani wa asilimia 50 kwa kipindi cha mwaka 2016/2017,ambapo pia
upatikanaji wa dawa umeongezeka katika vituo vya afya hadi kufikia asilimia 90
ikilinganishwa na asilimia 60 za hapo awali.
Amesema kuwa
mafanikio hayo yanatokana na juhudi za serikali kuongeza bajeti katika sekta ya
afya nchini kutoka kiasi cha shilingi trilioni 1.988 mwaka wa 2016/2017 hadi
kufikia trilioni 2.222 kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 ambapo ongezeko hilo ni
sawa na asilimia 11.77.
WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. MAJALIWA KASSIMU MAJALIWA AMESEMA SERIKALI ITAENDELEA KUPELEKA FEDHA KWENYE MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO.
Reviewed by safina radio
on
September 15, 2017
Rating:

No comments