CHELSEA YAMRUHUSU COSTA KUONDOKA
![]() |
DIEGO COSTAChelsea imekubaliana na Atletico Madrid kuhusu uhamisho wa mshambuliaji Diego Costa arudi Uhispania. |
Atletico imesema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye aliondoka katika klabu hiyo na kujiunga na Chelsea 2014 atafanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku chache zijazo.
Raia huyo wa Uhispania
hajaichezea Chelsea msimu huu na alitumia wakati mwingi wa mwezi Agosti akiwa
Brazil.
Hawezi kusajiliwa kama
mchezaji wa Atletico hadi mwezi Januari, wakati ambapo marufuku ya uhamisho
iliowekewa klabu hiyo itakamilika.
Timu hizo mbili zitakabiliana
Jumatano ijayo katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.
Costa ambaye ni mzaliwa wa
Brazil alijiunga na Chelsea kutoka Atletico Madrid kwa kitita cha £32m miaka
mitatu iliopita.
Alifunga mabao 58 katika
mechi 120 za Chelsea ikiwemo mechi 10 za ligi ya Uingereza msimu uliopita
ambapo Chelsea ilibuka mshindi.
CHELSEA YAMRUHUSU COSTA KUONDOKA
Reviewed by safina radio
on
September 22, 2017
Rating:

No comments