WATU SABINI WAMEUAWA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA MASHAMBULIZI MAWILI YA KUJITOA MUHANGA NCHINI IRAQ .
TAREHE 15-09-2017
![]() |
PICHA YA SHAMBULIZI LA KIGAIDI |
Kundi
linalojiita Dola la Kiislamu , limedai kuhusika na mashambulizi mawili ya
kujitoa muhanga nchini Iraq ambapo watu 70 wameuwawa na wengine wengi
wamejeruhiwa.
Maafisa
nchini humo wamesema idadi ya watu waliouwawa huenda ikapanda kutokana na watu
wengi waliojeruhiwa kuwa katika hali mbaya .
Washambuliaji
walishambulia hoteli pamoja na kituo cha polisi cha upekuzi karibu na mji wa
kusini mwa Iraq wa Nasiriyah siku ya Alhamis,ambapo Mahujaji kadhaa wa Iran ni
miongoni mwa waliouwawa.
Hata hivyo eneo
lililoshambuliwa liko katika barabara kuu inayotumiwa na mahujaji wa Kishia na
watu wanaotembelea eneo hilo kutoka magharibi mwa Iran kusafiri kwenda katika
miji mitakatifu ya Najaf na Karbala upande wa kaskazini.
WATU SABINI WAMEUAWA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA MASHAMBULIZI MAWILI YA KUJITOA MUHANGA NCHINI IRAQ .
Reviewed by safina radio
on
September 15, 2017
Rating:

No comments