WATU WATATU AKIWEMO AFISA WA POLISI WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA KIGAIDI HUKO AFGHANISTAN
TAREHE 14-09-2017
![]() |
WANAJESHI WAKIWA KATIKA MJI MKUU WA AFGHANISTAN KABUL |
Mshambuliaji wa kujitoa muhanga amejilipua karibu na uwanja wa mchezo wa kriketi katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul na kuua watu watatu akiwemo afisa wa polisi.
Duru za polisi zinasema watu wengine watano
walijeruhiwa katika shambulizi hilo wakiwemo maafisa wawili wa polisi.
Mshambuliaji
huyo alijilipua baada ya kusimamishwa katika kituo cha upekuzi na maafisa wa
polisi waliomshuku wakati alipokuwa akitembea kuelekea uwanja huo ambako mechi
ilikuwa ikiendelea.
Hata hivyo kitengo
cha Kundi la dola la kiislamu katika mkoa wa Khorasan kimedai kuhusika na
hujuma hiyo.
WATU WATATU AKIWEMO AFISA WA POLISI WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA KIGAIDI HUKO AFGHANISTAN
Reviewed by safina radio
on
September 14, 2017
Rating:

No comments