RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP ASAINI SHERIA MPYA YA KUONGEZA VIKWAZO DHIDI YA KOREA YA KASKAZINI
![]() |
RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP |
Waziri wa fedha wa Marekani ameidhinisha vikwazo hivyo dhidi ya makampuni ya fedha yanayofanya biashara zake ndani ya Korea Kaskazini.
Rais Trump pia amesema kuwa Benki Kuu ya Uchina iliagiza benki nyingine za Uchina kuacha kufanya biashara na Korea Kaskazini.
Hatua hii inakuja katika kipindi cha chini ya wiki mbili baada ya Umoja wa Mataifa kuidhinisha vikwazo vipya dhidi ya taifa hilo kwasababu ya jaribilo lake la hivi karibuni la nyuklia.
Hali ya wasiwasi imetanda katika kipindi cha wiki za hivi karibuni kutokana na hatua ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu, licha ya shinikizo kutoka kwa mataifa tajiri zaidi duniani.
RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP ASAINI SHERIA MPYA YA KUONGEZA VIKWAZO DHIDI YA KOREA YA KASKAZINI
Reviewed by safina radio
on
September 22, 2017
Rating:

No comments