KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAISHAURI SERIKALI KUWEKA ALAMA YA UTAMBUZI KATIKA MIRADI YAKE


tarehe 22-09-2017



Kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu imeishauri serikali kuweka alama ya utambuzi kwenye miradi yake yote wanayoijenga ili wananchi waweze kufahamu kazi inayofanywa na serikali yao.

Kamati hiyo imetoa kauli hiyo wakati baada ya kutembelea  miundombinu ya mawasiliano katika wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ili kuona maendeleo yake lengo likiwa ni kuhakikisha miradi hiyo ikiwemo ya mawasiliano inakamiliaka  kwa wakati ili wananchi waweze kupata mawasiliano.

Akizungumza wakati mara baada ya kutembelea miradi hiyo,makamu mwenyekiti wa wa kamati hiyo Mh Juma Kakoso,amesema kuwa pale serikali itakapoweka alama za utambuzi katika miradi yake itasaidia wananchi kuona kazi kubwa inayofanywa na serikali yao katika kuwaletea maendeleo ikiwemo miundombinu ya minara ya mawasiliano ya simu.


Kwa upande wake katibu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote Justina Mashiba amesema kuwa zaidi minara mia nne hapa nchini inafanya kazi ili kusaidia upatikanaji wa mawasiliano kwa wananchi na uwekaji wa alama za utambuzi umekwishaanza.
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAISHAURI SERIKALI KUWEKA ALAMA YA UTAMBUZI KATIKA MIRADI YAKE KAMATI   YA   KUDUMU  YA  BUNGE  YA  MIUNDOMBINU   YAISHAURI    SERIKALI  KUWEKA  ALAMA   YA  UTAMBUZI    KATIKA   MIRADI  YAKE Reviewed by safina radio on September 22, 2017 Rating: 5

No comments