SERIKALI KUTAFUTA WAWEKEZAJI KUJA KUWEKEZA KWENYE ZAO LA TANGAWIZI
TAREHE 14 -09-2017
![]() |
ZAO LA TANGAWIZI |
Ili
kuhakikisha kuwa zao la tangawizi linapata soko hapa nchini na nje ya nchi
serikali imesema kuwa inaendelea
kuhamasisha na kushawishi sekta binafsi kuja kuwekeza katika zao la viungo
ikiwemo tangawizi pamoja na kutafuta wateja wa zao hilo kupitia maonesho
mbalimbali ya kibiashara.
Hayo yamesemwa
leo bungeni mjini Dodoma na waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji Mh Charles
Mwiijage wakati akijibu swali la mbunge wa kuteuliwa Mh Anna Kilango Malechela
aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kutafuta soko la tangawizi ili
wananchi wanaolima zao hilo wapate sehemu kuuzia.
Mh Mwiijage
ameongeza kuwa ili kuhakikisha bidhaa ya tangawizi inayouzwa katika soko la
ndani la nje inakidhi ubora unaotakiwa serikali imejenga maabara ya chakula
yenye hadhi ya kimataifa ili kuwawezesha wazalishaji wa zao hilo kufikia
viwango vinavyotakiwa na masoko ya nje.
Ameongeza
kuwa mpaka sasa kuna makampuni 21 ambayo yanajishughulisha na shughuli za
uuzaji viungo nje ya nchi ikiwemo tangawizi,hivyo juhudi za serikali ni kuona
kuwa makampuni hayo yanakuwa na uwezo wa kuuza bidhaa hiyo ndani na nje ya nchi
ili kuinua uchumi wa taifa na wa mkulima.
SERIKALI KUTAFUTA WAWEKEZAJI KUJA KUWEKEZA KWENYE ZAO LA TANGAWIZI
Reviewed by safina radio
on
September 14, 2017
Rating:

No comments