WANAWAKE NCHINI SAUDIA ARABIA KUPEWA LESENI ZA KUENDESHA MAGARI.
TAREHE 27-09-2017
Vyombo vya
habari vya serikali ya Saudi Arabia vimeripoti kuwa kuanzia Juni mwakani
wanawake nchini humo watapewa leseni za kuendesha magari ambazo zitawawezesha
kuendesha magari kwa mara ya kwanza katika taifa hilo la kifalme.
Chombo
maalumu cha kiserikali kinatarajiwa kuundwa ndani ya siku 30 ili kutekeleza
amri hiyo ifikapo Juni 2018.
Wakati huohuo balozi wa Saudi Arabia kwenye
Umoja wa Mataifa mwana wa mfalme Khaled bin Salman amewaambia waandishi wa
habari kuwa wanawake hawatakuwa na ulazima wa kuwa na mtu ndani ya gari kwa
ajili ya kuwasimamia wakati watakapokuwa wanaendesha magari.
Amesema kuwaruhusu wanawake kuendesha magari
ni hatua kubwa nchini humo,ambapo Saudi Arabia ni nchi pekee ulimwenguni ambayo
wanawake hawaruhusiwi kuendesha magari.
WANAWAKE NCHINI SAUDIA ARABIA KUPEWA LESENI ZA KUENDESHA MAGARI.
Reviewed by safina radio
on
September 27, 2017
Rating:

No comments