TAREHE 21-09-2017
![]() |
MSHAMBULIAJI WA REAL MADRID CHRISTIANO RONALDO |
Antonio
Sanabria alifunga bao la ushindi kunako dakika ya 94 huku Real Betis
ikiishangaza Real Madrid na kupata ushindi katika uwanja wa Bernabeu kwa mara
ya kwanza katika ligi ya Uhispania La Liga katika kipindi cha miaka 19 .
Mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 21 aliruka na kufunga kichwa kizuri kufuatia krosi iliopigwa na Antonio
Barragans.
Kikosi cha Zinedine Zidane
kilitawala kipindi kirefu cha mechi, lakini Cristiano Ronaldo ni miongoni mwa
wachezaji wa nyumbani waliopoteza fursa za kuiweka mbele Real Madrid huku klabu
hiyo ikishambulia mara 27 bila kufaulu.
Hatua hiyo sasa inawawacha
mabingwa hao wa Ulaya wakiwa pointi saba nyuma ya viongozi wa ligi Barcelona.
Ronaldo ambaye alikuwa
amerudi kutoka kwa marufuku ya mechi tano alikuwa anashiriki katika mechi yake
ya kwanza ya ligi msimu huu .
Mshambuliaji wa Wales Gareth
Bale alimpatia Ronaldo fursa kabambe zaidi ili kuiweka mbele Real Madrid kwa kupiga
krosi ya chini lakini mchezaji huyo wa miaka 32 akashindwa kucheka na wavu.
Luka Modric mapema alikuwa
amepiga upande wa neti ya goli baada ya kutamba na mpira akiwa pekee huku
shambulizi la Bale likiokolewa.
Na huku wakiendelea kutawala
mechi, safu ya ulinzi ya Real Madrid ilipatikana imelala wakati bao la Sanabria
lilipokataliwa na refa.
Muda mfupi baadaye kinda huyo
wa zamani wa Barcelona hakufanya makosa wakati ambapo aliipata ngome ya Real
Madrid ikiwa imezubaa na hivyobasi kufunga bao la ushindi na hivyobasi kuiweka
Betis katika nafasi ya sita

No comments