WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS UTUMISHI NA UTAWALA BORA MH. ANGELA KAIRUKI AMESEMA ILI KUHAKIKISHA FEDHA ZA TASAF ZINANUFAISHA WALENGWA SERIKALI IMEONDOA KAYA ZAIDI YA ELFU 76



TAREHE 15-09-2017


WAZIRI  WA NCHI OFISI YA RAIS  NA UTAWALA  BORA MH. ANGELA KAIRUKI




Waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi na utawala bora Mh Angela Kairuki amesema kuwa ili kuhakikisha fedha zinazotolewa na mfuko wa kuhudumia kaya maskini yaani TASAF inawanufaisha walengwa,serikali imefanikiwa kuondoa zaidi ya kaya elfu 76 ambazo ziliingizwa kimakosa katika mfuko huo.

Mh Kairuki ameyaseam hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu Mh Nuru Fadhili aliyetaka kujua serikali inachukua hatua gani kwa kaya zinazohudumiwa na mfuko huo wa TASAF na wakati hawastahili kuwepo katika orodha ya kuhudumiwa kama watu maskini.

Amesema kuwa moja ya sababu inayosababisha kaya ambazo hazistahili kuingizwa kwenye orodha ya kuhudumiwa na TASAF ni kutokana na itikadi za kisiasa kutumika katika mikutano mikuu ya vijiji ambayo ndiyo inayorodhesha kaya hizo.

Kutokana na taizo hilo Mh Kairuki amewaomba wananchi pamoja na viongozi wa vijiji kushirikiana na serikali katika kuwabaini wale wote waliorodheshwa kimakosa katika mfuko huo ili waweze kuondolewa ili kaya zinazostahili ziweze kupata fedha hizo zitakazosaidia kuwapunguzia hali ya umaskini waliyonayo.

Hata hivyo tangu mfuko wa kuhudumia kaya maskini TASAF uanzishwe mwaka wa 2000 imefanikiwa kuwasaidia watu wenye hali ya umaskini kupata huduma za afya,elimu,maji,barabara na chakula.








WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS UTUMISHI NA UTAWALA BORA MH. ANGELA KAIRUKI AMESEMA ILI KUHAKIKISHA FEDHA ZA TASAF ZINANUFAISHA WALENGWA SERIKALI IMEONDOA KAYA ZAIDI YA ELFU 76 WAZIRI  WA  NCHI  OFISI  YA  RAIS UTUMISHI  NA  UTAWALA  BORA MH. ANGELA  KAIRUKI AMESEMA  ILI KUHAKIKISHA  FEDHA ZA TASAF ZINANUFAISHA  WALENGWA   SERIKALI  IMEONDOA  KAYA ZAIDI YA ELFU  76 Reviewed by safina radio on September 15, 2017 Rating: 5

No comments