MKUU WA WILAYA YA LINDI SHAHIDI NDEMANGA AMEITAKA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA TRA KUDHIBITI NA KUCHUKUA HATUA KWA YEYOTE ATAKAYEINGIZA BIDHAA KWA KUPITIA BANDARI BUBU KATIKA WILAYA HIYO.










MKUU WA WILAYA  YA  LINDI BW. SHAHIDI NDEMANGA

Mkuu wa wilaya ya Lindi Shaidi Ndemanga ameitaka mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Lindi kudhibiti na kuchukua hatua kali mfanyabiashara yeyote atakayeingiza bidhaa kwa njia ya magendo kupitia bandari bubu zilizoko katika wilaya hiyo.

Bw Ndemanga ametoa kauli hiyo wakati wa operesheni maalumu ya kuzuia magendo iliyofanyika katika mwambao mwa bahari ya Hindi ,ambapo amesema kuwa bandari ambazo TRA inatakiwa kuzuia bidhaa za magendo kuingia ni bandari za Mchinga,Shuka na Sudi.

Amesema kuwa endapo TRA itazuia magendo hayo serikali itaweza kupata mapato mengi na wale watakaokamatwa wanajihusisha na biashara hiyo haramu watachukuliw hatua kali za kisheria ikiwemo kufungwa jela ili iwe fundisho kwa wengine.


Hata hivyo katika operesheni hiyo imekamatwa shehena mbalimbali za mizigo ikiwemo mifuko mia moja arobaini na tano ya sukari na madumu ya mafuta ya kupukia 76 yenye thamani ya shilingi milioni sita.
MKUU WA WILAYA YA LINDI SHAHIDI NDEMANGA AMEITAKA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA TRA KUDHIBITI NA KUCHUKUA HATUA KWA YEYOTE ATAKAYEINGIZA BIDHAA KWA KUPITIA BANDARI BUBU KATIKA WILAYA HIYO. MKUU   WA  WILAYA  YA LINDI  SHAHIDI  NDEMANGA  AMEITAKA   MAMLAKA  YA MAPATO TANZANIA  TRA  KUDHIBITI  NA KUCHUKUA  HATUA  KWA  YEYOTE  ATAKAYEINGIZA BIDHAA  KWA  KUPITIA  BANDARI  BUBU  KATIKA  WILAYA  HIYO. Reviewed by safina radio on September 15, 2017 Rating: 5

No comments