MKUU WA MKOA WA DAR -ES SALAAM PAUL MAKONDA AMEZIELEKEZA MANISPAA ZOTE ZA MKOA HUO KUTOA MIKOPO NAFUU KWA WAJASIRIAMALI
TAREHE 28-09-2017
![]() |
MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA |
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Paul Makonda amezielekeza manispaa zote
za mkoa huo kutoa mikopo nafuu kwa wajasiriamali wenye viwanda
vidogovidogo ili kuweza kusaidia katika uanzishwaji wa viwanda
mkoani humo
Bw Makonda ametoa agizo hilo
jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari
namna alivyojipanga kusaidia wananchi wake kiuchumi,ambapo amesema kuwa kuna
asilimia kumi za fedha katika kila manspaa za mkoa huo tano kwa ajili ya akina
mama na tano kwa ajili ya vijana hivyo watatumia fedha hizo ili waweze
kuanzisha viwanda vidogovidogo.
Amesema kuwa amefanya mzungumzo na mfuko wa hifadhi ya jamii
NSSF ili kuweza kutoa mikopo nafuu na kusaidi wafanya biashara katika
kuanzisha viwanda vidogovidogo na kuwa taka wafanya biashara hao kufika
ofisi ya mkoa kujiandisha ili wapewe mikopo hiyo.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa ataanzisha soko la kuuza bidhaa
zilizotengenezwa na viwanda vya ndania jijini Dar es salaam hivyo,amewataka
wamachinga kuuza bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili kukuza uchumi wa taifa
na kuongeza ajira kwa watanzania haswa vijana.
MKUU WA MKOA WA DAR -ES SALAAM PAUL MAKONDA AMEZIELEKEZA MANISPAA ZOTE ZA MKOA HUO KUTOA MIKOPO NAFUU KWA WAJASIRIAMALI
Reviewed by safina radio
on
September 28, 2017
Rating:

No comments