SERIKALI KUENDELEA KUZIJENGEA UWEZO TAASISI ZA UONGOZI HAPA NCHINI
tarehe 22-09-2017
![]() |
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS NA UTAWALA MH. ANGELA KAIRUKI |
Waziri wa
nchi ofisi ya rais utumishi na utawala bora Mh Angela Kairuki amesema
kuwa,serikali itaendelea kuzijengea uwezo taasisi za uongozi nchini ili ziweze
kutoa mafunzo kwa viongozi wa kada mbalimbali kwa lengo la kuharakisha
maendeleo ya taifa.
Mh Kairuki
ameyasema hayo jijini Dar-es-salaam wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya taasisi
ya viongozi nchini,ambapo amesema kuwa zaidi ya viongozi elfu moja na mia saba
wamepata mafunzo kutoka taasisi ya uongozi, mafunzo ambayo yamewajengea ufanisi
katika utendaji wao wa kazi.
Amesema kuwa
serikali imeingia mkataba wa miaka minne na serikali ya Finland katika
kuboresha utendaji wa taasisi hiyo kwa lengo la kuwandaa viongozi watarajiwa
watakaokuwa na weledi katika utendaji wao wa kazi.
Hata hivyo
waziri Kairuki amesema serikali ina mango wa kuandaa tovuti maalumu ya kuratibu
majina ya viongozi watakaokuwa tayari kushika nyadhifa mbalimbali serikalini
pale watakapohitajika.
SERIKALI KUENDELEA KUZIJENGEA UWEZO TAASISI ZA UONGOZI HAPA NCHINI
Reviewed by safina radio
on
September 22, 2017
Rating:

No comments