WATU 8 WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE 12 KUJERUHIWA NCHINI MAREKANI.
TAREHE 1-11-2017

Shambulizi Meya wa mji wa New York, Bill De Blasio, amesema kwamba watu 8 wamefariki
dunia na zaidi ya 12 wamejeruhiwa baada ya
gari kuwagonga waendesha baiskeli mjini humo.

Kwa upande wake Kamishna
wa polisi wa jiji la New York, James O'Neill, amemuelezea mtu aliyetekeleza
tukio hilo kuwa ni kijana wa miaka 29 aliyekuwa anaendesha gari ndogo la
kubebea mizigo alilokuwa amelikodi.
O`Nell Amesema gari
hilo liliwagonga watembea kwa miguu na wapanda baiskeli kabla ya kugongana na
basi la shule.
Polisi mjini humo
wametoa tamko kwamba wanalichukulia tukio hilo kama shambulizi la kigaidi ,
Mtuhumiwa wa tukio hilo amechukuliwa na polisi kwa mahojiano zaidi katika kituo cha Lower Manhattan.
Hata hivyo Vyombo vya
habari nchini Marekani vimenukuu taarifa za polisi kuwa kijana huyo aliamua
kuendesha gari hilo katika njia ya waendesha baisikeli iliyoko karibu na Mto
Hudson eneo la Lower Manhattan ya chini ,kabla ya kupigwa risasi na maafisa wa
polisi ili kuzuia shambulio alilolipanga.
WATU 8 WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE 12 KUJERUHIWA NCHINI MAREKANI.
Reviewed by safina radio
on
November 01, 2017
Rating:
No comments