NADAL KULIPWA DOLA ZA KIMAREKANI ELFU 14 KAMA FIDIA

Rafael Nadal anashikilia namba moja kwa ubora duniani
Image caption
Mahakama mjini Paris imemuamuru waziri wa michezo wa Ufaransa Roselyne Bachelot kumlipa mcheza tennis nyota Rafael Nadal kiasi cha dola za kimarekani 14,000 kutokana na kumtuhumu kutumia dawa zilizokataliwa michezoni.
Nadal alimfungulia mashitaka kwa kauli yake hiyo kwa kusema imemuharibia taswira yake kwa jamii.
Awali Nadal alitaka dola laki moja lakini kutokana na ushauri wa watu akaamua kupunguza.
Mchezaji huyo namba moja duniani amesema fedha hizo atazitumia kusaidia wasiojiweza nchini Ufaransa.
NADAL KULIPWA DOLA ZA KIMAREKANI ELFU 14 KAMA FIDIA NADAL KULIPWA DOLA ZA KIMAREKANI ELFU 14 KAMA FIDIA Reviewed by safina radio on November 17, 2017 Rating: 5

No comments