MAREKANI YAIONYA KOREA KASKAZINI
TAREHE 30-11-2017
Marekani imeuonya
utawala wa Korea Kaskazini kuwa utaangamizwa kabisa iwapo vita vitazuka baada
ya Korea Kaskazini hapo jana kurusha kombora la masafa marefu ambalo
lilisemekana lina uwezo wa kufika kokote nchini Marekani.
Akizungumza katika
mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, balozi wa Marekani
katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley amesema hawajawahi kutafuta kuingia vitani
na Korea Kaskazini, lakini iwapo vitazuka, itakuwa ni kutokana na vitendo vya
kichokozi kama walivyoshuhudia jana hali inayoweza kuifanya nchini hiyo
kusaharibiwa kabisa.
Naye waziri wa
Mambo ya Nje wa Ujerumani, Sigmar Gabriel amesema Korea Kaskazini imekiuka
sheria za kimataifa na kwamba vitendo hivyo vinatishia usalama wa kimataifa.
Kwa upande wake rais
wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema anatumai China na Urusi zitaiongezea Korea
Kaskazini vikwazo ili kuishinikiza kuachana na mpango wake wa kinyuklia na
kurusha makombora.
MAREKANI YAIONYA KOREA KASKAZINI
Reviewed by safina radio
on
November 30, 2017
Rating:

No comments